Friday, July 10, 2015

RAIS Kikwete afunga rasmi Bunge


Bunge la Tanzania

 RAIS  Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania, jana jioni alifunga rasmi bunge la 10 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania huku idadi kubwa ya wapinza wakisusia sherehe hizo.

Wapinzani nchini Tanzania wamesusia hotuba ya Rais Kikwete ya kuvunja bunge hilo kama njia ya kuwaunga mkono wenzao 32 waliofukuzwa bungeni baada ya kuupinga vikali muswada wa mafuta na gesi wakidai umewasilishwa kinyemela kwenye bunge hilo.
Wakati wa kulifunga bunge hilo hiyo jana, Rais Jakaya Kikwete alihusisha sehemu kubwa ya hotuba yake katika mambo aliyosema ni mafanikio ya serikali yake tangu alipoingia Ikulu mwaka 2005. Hata hivyo amekiri kuwa ameshindwa kulifufua Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). Ingawa wapinzani wanaendelea kulalamikia, lakini Rais Kikwete ametoa sifa nyingi kwa Spika wa bunge hilo Anne Makinda. Amewashukuru pia wabunge, viongozi mbalimbali wa Serikali, wananchi na chama chake akisisitiza kuwa anaondoka madarakani akiicha Tanzania ikiwa salama. Hata hivyo wakati wakihojiwa kuhusu utendaji kazi wa bunge hilo la 10, wabunge mbalimbali wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wamekuwa na maoni tofauti, huku baadhi yao wakisema halikuwa na mafanikio zaidi

No comments:

Post a Comment