![]() |
| Waislamu wa nchini Marekani |
Taasisi ya Misaada ya Kiislamu ya Marekani imeandaa chakula kwa watu maskini nchini humo katika miji 20 tofauti bila ya kujali dini zao, ikiwa ni kuonesha kuwa, mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa kupendana na kuhurumiana.
Shirika la habari la RASA limeripoti habari hiyo leo na kumnukuu mkurugenzi wa mradi huo akisema kuwa, kuwasaidia maskini na wasiojiweza ni katika sifa za kimaanawi za mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo, misafara mbalimbali ya chakula ya taasisi hiyo imetumwa kwenye miji 20 ya Marekani ikiwa na vyakula. Amesema, zaidi ya familia milioni 17 za Marekani zina shida ya chakula, na ndio maana Waislamu wa nchi hiyo wameamua kuitumia fursa hii ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kugawa chakula katika miji hiyo 20 ya Marekani.
Mipango hiyo iliwasilishwa na serikali Athens Alhamisi usiku kwa matumaini ya kupata mkopo mpya kukwepa kufilisika.
Mageuzi hayo yanakaribiana na wanayotafuta wakuu wa shirika la fedha la kimataifa IMF, Umoja wa Ulaya na benki kuu ya Ulaya -- wanaojadili mpango huo kupitia njia ya simu.
Bunge la Ugiriki linatarajiwa kupigia mapendekezo hayo kura.
Lakini licha ya yatakayofikiwa, waziri mkuu wa Ugiriki, Alexis Tsipras anaonekana kurudi nyuma.
Hatua alizokubali zinaambatana na kupandisha kodi, kupunguza mishahara ya wafanyakazi wa umma na kuzidisha ubinafsishaji.

No comments:
Post a Comment