Rmadhan Ally Kingalu |
RAIS Jakaya
Kikwete (2/7/15)leo anataraji kuungana na wakazi wa mkoa wa Morogoro katika
mazishi ya Chifu Kingalu Mwanabanzi wa 14 Ramadhan Ally Machanga Kingalu
aliyefariki dunia jana katika hospitali ya Rufani Muhimbili Jijini Dar es
salaam.
Kwa mujibu wa mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Rajabu Rutengwe,mazishi
hayo yanataraji kufanyika leo saa 7 mchana baada ya sala ya Adhuhuri huku
nyumbani kwake katika kijiji cha Kinole wilayani Morogoro.
Dk Rutengwe alisema Mwanabanzi wa 14 alikuwa akisumbuliwa na
ugonjwa wa Shikizo la damu na kisukari kwa muda mrefu ambapo 26.6.2015
alikimbizwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro na baadae kuhamishiwa
Muhimbili kwa matibabu.
"mwili wake umesafirishwa moja kwa moja kutoka jijini Dar es
salaam tangu jana hadi kijijini Kinole na wageni walianza kuwasili tangu jana
kijijini huko kwa mazishi"alisema
Akiwataka wanachi wa mkoani humo kuungana na ugeni wa kitaifa
katika mashishi hayo, Dk Rutengwe aliwataka viongozi mbalimbali wa
makampuni,mashirika,taasisi mbalimbali zikiwemo za dini na taaluma kuungana kwa
pamoja katika safari hiyo ya mwisho.
No comments:
Post a Comment