Polisi wakiwa katika eneo la ajali , Kondoa wilayani Kilosa |
WATU wanne wamefariki dunia na 31 kujeruhiwa baada ya basi
aina ya Isuzu Journey T837 TM kuigonga treni ya mizigo iliyokuwa ikitoka Mkoani
Morogoro kuelekea wilayani Kilosa maeneo ya Chek-line wilaya ya Kilosa,mkoani Morogoro.
Kwa mujibu wa abilia waliuonusurika
katia ajari hiyo Maurid Yahaya(35) wa kichangani,Hasan Kikudo kondakita wa basi
na Martina Kabete (59)mkazi wa jijini Dar es salaam ajali hiyo ilitokea saa
1.30 asubuhi wakati wakijaribu kukatisha kwenye reli na basi hilo.
"ilikuwa asubuhi tukitokea
kijiji cha Tindiga kuelekea mjini Morogoro,tulipofika eneo la Kibaoni kuna
makutano na reli sasa nadhani dereva hakujua kama kuna treni inakuja tulipofika
katikati ya reli ghafla treni ikatugonga na kuburuzwa...kwa haraka haraka
nadhani watu kama saba wamekufa"alisema Martina.
Hata hivyo majeruhi hao
waliokimbizwa katika hospitali ya Rufaa mkoani Morogoro na kulazwa wodi namba 1
na 3 walisema treni hiyo ilisimama na kuwapakia majeruhi na waliokufa kisha
kuwapeleka Kilosa mjini ambako walikimbizwa hospitali ya wilaya kwa huduma za
kitabibu.
Akizungumza na waandishi wa habari
Kaimu kamanda wa polisi mkoani Morogoro Musa Malambo alisema ajali hiyo
ilitokea eneo hilo la Kibaoni ikihusisha basi la kampuni ya Huwel kutoka
Tindiga kuelekea mjini Morogoro kushindwa kusimama na kuligonga Treni.
Alisema katika ajari hiyo
ilisababisha vifo vya watu wanne hapohapo waliotambuliwa kwa majina
wakiwemo wanaume wawili na wanawake wawili ambao ni Salehe
Ngombaiko(35),Husna(33),Sulati Mwajiri(6)na Mwajiri(35).
Akifafanua juu ya majeruhi wa ajali hiyo kaimu Kamanda Malambo
alisema kati ya majeruhi 31 watu 10 ni wanaume,15 ni wanawake ambapo 6 ni
watoto na kwamba wote wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kilosa.
Katika ufafanuzi wake Kaimu kamanda huyo aliwataja madereva wa
basi kuwa ni Bakari Nyange mkazi wa Kilosa na dereva wa treni No 88 U3 ilikuwa
ikiendeshwa na Inea Chipandula(48) mkazi wa Morogoro.
No comments:
Post a Comment