![]() |
| Dk Binilith Mahenge(wakwanza kushoto) akiwa na waandishi wa habari |
WADAU wa mazingira wameipongeza hatua iliyochukuliwa na Waziri
ofisi ya Makamu wa Raisi (mazingira)Dk Binilith Mahenge kwa kufunga viwanda
visivyozingatia kanuni na taratibu za uhifadhi na utunzaji wa mazingira .
Wakiongea na Dira ya Mazingira jijini
Dar es salaam mapema leo, baadhi ya wananchi wamesema kuwa, zoezi hilo liwe
endelevu ikiwa ni pamoja nakufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kulinda afya za
wafanyakzi na wananchi wanaoishi jirani na viwanda.
Wamesema , hatua hiyo ya waziri anayehusika
na Mazingira kufanya ziara za kustukiza na kutoa agizo la kusimamisha shughuli
za uzalishaji kwa viwanda visivyozingatia sheria, kanuni na taratibu za
uhifadhi wa mazingira kwa kiasi fulani zinaonesha uwajibikaji.
Hivi karibuni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu
wa Rais (Mazingira), Dk Binilith Mahenge amekifungia Kiwanda cha kuzalisha
mafuta ya kula cha Murzal Oil Limited kwa muda usiojulikana baada ya kukaidi
agizo lililotolewa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira
(NEMC).

No comments:
Post a Comment