RAIS Jakaya Kikwete amesema serikali itaendelea kuheshimu
uongozi wa jadi nchini kwakua kufanya hivyo kunaimarisha na kuiwezesha serikali
kutekeleza kwa urahisi majukumu yake ya utawala.
Rais Kikwete alisema hayo juzi
kwenye mazishi ya Chifu Kingalu Mwanabanzi wa 14 Ramadhan Ally Machanga Kingalu
yaliyofanyika nyumbani kwake chifu huyo katika kijiji cha Kinole wilayani
Morogoro.
Katika salamu za lambilambi kwa
wanachi wa mkoa huo wa Morogoro na wageni kutoka sehemu mbali mbali ndani na
nje ya nchi Rais Kikwete alisema lengo kubwa la kuendeleza ushirikiano na
viongozi hao wa kijadi ni kuimalisha amani,usalama na utulivu wa nchi.
"marehemu Chifu Machanga
Kingalu 14 alikuwa msaada mkubwa katika utatuzi wa migogoro mbalimbali ikiwemo
ya kijamii hususani ya wakulima na wafugaji na amekuwa mstari wa mbele
kuhakikisha mazingira hayaharibiwi akihimiza kupanda miti na kuilinda katika
maeneo mengi mkoani hapa"alisema Kikwete.
Aidha aliahidi kutafutia ufumbuzi wa
changamoto ya matimizi ya nyara za serikali ikiwemo matumizi ya ngozi za
wanyama katika shuguli za viongozi wa jadi kote nchini ili kuwawezesha kufanya
kazi zao kwa ufanishi na manufaa ya taifa kwa jumla.
Sambamba na mazishi hayo rais Kikwete
akiwa na Mkewe Salma Kikwete pia alishuhudia zoezi la kumsimika chifu mpya
kingalu wa 15 Husein Ali Machanga ambaye ni mdogo wake marehemu Ramadhani Ali
machanga Kingalu wa 14.
Baada ya kula kiapo chifu mpya
kigalu wa 15 Husen Ali alimwomba Rais Kikwete kuharakisha kupatikana ufumbuzi
wa machifu kupata kibali cha matumizi ya vifaa vitokanavyo na wanyama ili
waweze kuwatumikia wanachi kwa faida ya taifa.
"tofauti na zamani sasa hivi
viongozi wa mila tunabanuwa na sheria zilizopo na kutufanya kushindwa
kutekeleza majukumu yetu ya kimila kutokana na kukosa baadhi ya vifaa vya
kutumia zikiwemo ngozi za wanyama pori kama Chui,Simba,Kenge na
Mamba...tunaomba kupata kibali hata kwa kiwango fulani na Muda
maalumu"alisema Chifu kingalu 15.
Chifu Kingalu Mwanabanzi wa 14
Ramadhan Ally Machanga Kingalu alifariki dunia Julai mosi katika hospitali ya
Rufani Muhimbili Jijini Dar es salaam akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukali na
shinikizo la damu.

No comments:
Post a Comment