Wednesday, July 29, 2015

TAMASHA la wasanii duniani laanza nchini Senegal

WASANII wa tasnia ya filamu kutoka nchi mbalimbali duniani wameanza kuwasili mji mkuu wa Senegal, Dakar kwaajili ya maandalizi ya tamasha la kila mwaka lijulikanalo kama Forum street Festival.
Kupitia tamasha kama hilo wasanii wanapata fursa kuwasilisha ujumbe uliopo mioyoni mwao na kutengeneza majadiliano yanayoangazia masuala mbalimbali katika jamii

Ni katika shule moja maarufu iliyopo kwenye kitongoji cha mji wa Dakar , madarasa ya shule hii ambapo kwa sasa yamegeuka kuwa kumbi za tamasha hilo,huku viti na meza vikiwa vimewekwa kando,vijana wamekaa chini kwa umakini mkubwa wakiendelea na michezo mbali mbali ya kuigiza

No comments:

Post a Comment