TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwa kushirikiana na
Wakurugenzi wa Manispaa za jiji la Dar es Salaam wanaendelea kushughulikia
changamoto mbalimbali zilizojitokeza kwenye baadhi ya vituo kufuatia mashine za
BVR kushindwa kufanya kazi vizuri.
Hayo yamebainishwa mapema leo na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam bwana Said Mecky Sadiki wakati akiongea na waandishi wa habari.
Amesema kuwa
kumekuwa na malalamiko yanayotolewa na wananchi yanayosababishwa na
waandikishaji kuchelewa kufika katika vituo walivyopangiwa na kusababisha
wananchi kusubiri muda mrefu bila kuandikishwa.
Amesisitiza kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua kali kwa yeyote atakayebainika kuhusika na uzembe huo.
Amewaagiza Wakurugenzi wa Manispaa zote za jiji la Dar es Salaam kuwafuta kazi watendaji wazembe ili kuepusha madhara na vurugu zinazoweza kuepukika.

No comments:
Post a Comment