Wednesday, March 30, 2016

KENYA yaruhusu wakinamama kwenda kazini na watoto

KENYA imeruhusu akina mama wanaonyonyesha kwenda na watoto wao kazini kufuatia bunge la nchi hiyo kupitisha muswada wa afya.

Muswada  huo wa afya unazitaka kampuni kutenga maeneo maalumj ya kuwanyonyesha watoto ambayo yatakuwa na mashine ya kukamua maziwa ya mama,jokovu la kuhifadhi maziwa na chakula na kuhakikisha mandhari sawa ya a watoto wachanga .
Maeneo hayo maalum yatakuwa na mashini ya kukamua maziwa ya mama, jokovu la kuhifadhi maziwa na chakula cha watoto pamoja na kuhakikisha mandhari sawa ya watoto wachanga.
Chini ya mswada huu waajiri lazima watoe muda kwa wanawake kuwanyonyesha watoto hao, kwa kupokezana.
Rachel Nyamai, mbunge aliyewasilisha mswada huo amesema utasaidia wanawake kufanya kazi vyema na wakati huohuo kuimarisha afya ya mtoto.







No comments:

Post a Comment