Wednesday, March 30, 2016

SERENGETI Boys kucheza mchezo wa kirafiki na vijana Misri

Timu ya Taifa ya vijana ya Tanzania 
TIMU  ya Taifa ya Vijana Tanzania inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki na timu ya Taifa ya vijana ya Misri.
Mchezo wa kwanza kati ya Serengeti Boys ya Tanzania dhidi ya The Pharaohs ya Misri utachezwa siku ya Jumamosi, Aprili 2 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo wa pili utachezwa Jumanne Aprili 5 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Msafara wa The Pharaohs unatarajiwa kuwasili Alhamis tarehe 31, Machi ukiwa na watu 33, wakiwemo wachezaji 25 pamoja na viongozi 8, na wataondoka nchini tarehe 6 Aprili kurudi kwao nchini Misri.
Kikosi cha Serengeti Boys kinachonolewa na makocha Bakari Shime na Sebastian Mkomwa wakishauriwa na Jan Poulsen, kimeendelea na mazoezi katika uwanja wa Karume, zilipo ofisi za Makao za Makuu ya TFF.









No comments:

Post a Comment