![]() |
| Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan |
MAKAMU wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan 18 aprili anatarajiwa
kuzindua mbio za mwenge wa Uhuru kwa kuuwasha katika uwanja wa Jamuhiri Mkoani
Morogoro.
Hayo yamebainishwa na
Mkuu mpya wa mkoa Dk. Kebwe Stephen wakati akizungumza na waandishi wa habari
mkoani hapa na kufafanua kuwa zaidi ya miradi 40 inataraji kupitiwa na
kuzinduliwa mkoani humo.
“Maanadalizi ya uzinduzi
huo yameanza kwa kuundwa kamati tisa (9) zizitakazofanikisha zoezi hilo kubwa
na lenye heshima katika mkoa wetu...Jukumu kubwa la Mkoa, pamoja na
majukumu mengine tuliyopewa ni kuhamasisha ushiriki wa wananchi na wadau
wengine kwa kutumia njia mbalimbali ikiwemo matangazo kupitia vyombo vya habar
tusaidieni”alisema Dkt Kebwe
Aidha Dkt. Kebwe ameagiza
Wakuu wa Wilaya za Mkoa huo ,Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za
Wilaya, miji midogo na Manispaa, pamoja na watendaji wote wa Serikali,
kuhakikisha wanasimamia kikamilifu maandalizi ya kufanikisha mbio za
Mwenge wa Uhuru katika Wilaya na Halmashauri zote pindi utakapofika katika
maeneo yao.
Kwa mjibu wa mkuu huyo
wa mkoa Kaulimbiu ya mbio za Mwenge huo wa Uhuru kwa mwaka huu kitaifa ni ,
“vijana ni nguvukazi ya taifa, washirikishwe na kuwezeshwa”.

No comments:
Post a Comment