Saturday, April 2, 2016

WAJAWAZITO Morogoro wajifungulia majumbani

UKOSEFU wa zahanati,vituo vya afya,hospitali  na vifaa tiba vijijini nchini unawalazimu wanawake wajawazito kata mpya ya Kibuko tarafa ya Mkuyuni wilayani Morogoro kujifungulia majumbani na njiani kwa vifaa vya jadi vikiwemo vibabazi vya miti na Majani kama mbadala wa wembe.


Hayo yalifahamika karibuni mbele ya timu ya waandishi wa habari iliyotembelea vijiji vya kata hiyo kwa ushirikiano na Mtandao wa jinsia nchini-TGNP kujionea na kuibua changamoto zinazowakabili wanachi na kumkuta mama jina tunalo(Pili Selemani(16)wa kitongoji cha Mngusi-Mwalazi aliyejifungulia njiani kwa vifaa hivyo.

Wakisimulia tukio hilo kwa nyakati tofauti baadhi ya mashuhuda Zena Ramadhan(48) na Mwanvua Ally(52) walisema wanalazimika kufanya hivyo nakuwa jambo la kawaida kutokana na matukio hayo kujitokeza mara kwa mara kwa kutokuwa karibu vituo vya huduma za afya,ukosefu maandalizi ya kutosha,umasikini na kuenea imani potofu.

“kibanzi hiki cha jani ndicho tumetumia kama wembe kukatia kitovu cha mtoto kumnusuru mama na mwanae baada ya mtoto kutoka...hii inatokana na kutokuwa na maandalizi ya vifaa vya kujifungulia.Sasa hivi tunaona kawaida hasa inapotokea tukachelewa hospitalini”alisema Mwanvua. 

Sambamba na hayo walisema wamekuwa hawafanyi maandalizi hayo ya ikiwemo kuwahi huduma za afya na kununua vifaa vya kujifungulia vikiwemo viwembe na glavuzi kutokana na imani kuwa ni kujitia mkosi wa kutojifungua salama na kupoteza mtoto pia kuwepo taarifa kuwa vifaa hivyo vinapatikana hospitalini bure.


Akizungumzia changamoto hiyo Mwenyekiti wa kijiji hicho cha Mwalazi Rajabu Ngevu alikili vitendo hivyo kujitokeza mara kwa mara kutokana na changamoto nyingi zikiwemo za umbali wa huduma ya Afya,umasikini,mapokezi duni katika vituo vya afya na tatizo la uduni wa miundombinu.


No comments:

Post a Comment