![]() |
| Papa wa kanisa katoliki Francis Paulo |
Mwongozo huo ume
kwenye waraka aliouandika akizingatia majadiliano ya mikutano miwili ya wakuu
wa kanisa hilo kuhusu sera, maarufu kama sinodi.
Waraka huo
ulisubiriwa sana na waumini takriban 1.3 bilioni wa kanisa hilo duniani.
Kicha cha waraka huo
ni "On Love in the Family" (Kuhusu Upendo katika Familia) na
haubadilishi mafundisho ya kidini ya kanisa hilo.
Lakini unafungua
njia kwa maaskofu katika kila nchi kufafanua mafundisho ya kidini ya kanisa
hilo kuambatana na utamaduni wa maeneo yao, mwandishi wa BBC anayeangazia
masuala ya kidini Caroline Wyatt anasema.
Papa Francis
amewahimiza mapadri kutumia hekima na busara wakishughulikia “familia
zilizoumizwa” na kuwa na huruma badala ya kutoa hukumu haraka.
Amekosoa ubinafsi
ambao anasema umewafanya watu wengi katika nchi za magharibi kuthamini sana
kutosheleza mahitaji yao binafsi badala ya mahitaji ya wake au waume zao katika
ndoa.
Huku akiunga mkono
kutolewa kwa elimu kuhusu ngono, amesema inafaa kuwa kwenye mfumo wa kutoa
elimu kuhusu upendo.
Amesisitiza sana
kuhusu ulezi wa kiroho na kuandaliwa vyema kwa watu kabla ya kufunganishwa
kwenye ndoa kuhusu mahitaji ya maisha katika ndoa.

No comments:
Post a Comment