![]() |
| Waziri wa Afya Ummy Mwalimu |
SERIKALI imezitaka Taasisi na ofisi
zote za umma na binafsi nchini kuweka hadharani namba za mawasiliano kwa
wananchi na kufungua vyumba na madirisha maalumu kwa wazee ili wahudumiwe
kikamilifu na kwa wakati.
Wito huo umetolewa kwa nyakati tofauti na waziri wa Afya,Maendeleo ya jamii,jinsia wazee na watoto Ummi
Mwalimu wakati akizungumza na wazee mkoani hapa sambamba na wafanyakazi wa
wizara hiyo hospitali ya rufaa mkoni Morogoro.
"haiingii akilini kuona wazee waliolitumikia taifa kwa
uadilifu muda mrefu na kuliletea maendeleo wakiendelea kutaabika kimaisha hasa
kwenye huduma ambazo ni muhimu na laziama kwao...naagiza taasisi ofisi za umma
na binafsi yakiwemo Mbenki,Tanesco,Mahospitali na mamalaka za maji kuwa na
vyumba au madirisha ya wazee"alisema Ummy.
kwa mujibu wa waziri Ummy Tanzania inawazee wenye miaka kuanzia 60
na kuendelea zaidi ya Mil.2.5 waliogawanyiaka kwa makundi likiwemo la wenye
miaka 60-64 niasilimia 31 ambao kwa namana moja ni wenye ahueni, 65-69 asilimia
20, miaka 70-74 asilimia 19 kundi inaanza kuteteleka huku wenye miaka 75-79
wakiishia asilimia 12 na miaka 80 kuendelea asilimia 19 kundi lililotaabani
kimaisha.
Akitoa salam za wazee mkoni humo Mkurugenzi wa asasi ya wazee mkoani hapa MOROPEO Samson Msemembo mbali na kumpongeza waziri kwamsimamo wake na juhudi za kuwaokoa wazee alimwahidi kuwa nyuma yake kwa changamoto zote zilizo mbele ya wazee kwa faida ya taifa.
“tumeshuhudi maneno mengi ikiwemo serikali sikivu,inajali katika
walatawala zilizopita lakini ukweli waziri labda serikali hii ndio mkombozi
wetu mana tumeshuhudia mambo mengi maana tumelia sana tulichoambulia ni ahadi
zisizotekelezeka…fikiria sera ya wazee inamiaka 13 hakuna lolote tuko nyuma
yako waziri”alisema Msemembo.
Aidha alimwomba waziri Ummi kuhakikisha wazee wanapata nafasi ya
uwakilishi katika vyombo mbalimbali vya maamuzi nchini kuanzia kijiji hadi
taifa sambamba na kuanza kulipwa pensheni ili wawe karibu na jamii kwa
kutekelezewa haraka mahitaji wanayoyahitaji kwa faida yao na vizazi vyao.

No comments:
Post a Comment