CHAMA cha waendesha pikipiki katika jimbo la Segerea (SEBOA)kinatarajia kuendesha semina ya wiki moja kwa madereva wa bodaboda na bajaji kwa lengo la kuwaweesha kuelewa na kupambana na mbinu za uhalifu.
Akiongea na Mbiu Media mapema leo, Mwenyekiti wa chama hicho Bwana Iddy Kilonzo Kikoti amsema kuwa semia hiyo itafanyika katia Ukumbi wa Rosehill uliopo Tabata Segerea jijini Dar es salaam na inatarajiwa kuanza tarehe 17 mwezi juni na kumalizika tarehe 30 mezi huohuo w a juni.
Amesema , wataalamu mbalimbali toka jeshi la polisi usalama wa raia na usalama barabarani. mamlaka ya mapato nchini, Sumatra, maafisa biashara wa manispaa zote za jiji la Dar es salaam,madaktari toka Hospitali ya Muhimbili kitengo cha mifupa cha MOI watatoa mada mablimbali kwa madereva hao.

No comments:
Post a Comment