Sunday, June 19, 2016

SHULE zatakiwa kuzalisha wasomi wa sayansi ili kukabiliana na changamoto za viwanda

Mkuu wa mkoa wa Morogoro Kebwe Stevenm Kebwe
SERIKALI mkoani Morogoro imeziagiza shule zote za sekondari mkoni humo kuelekeza nguvu katika masomo ya sayansi kwa wanafunzi wake ikiwa ni mkakati wake kuzalisha rasilimali watu  ili mkoa huo ulikabili soko la ajira kutokana na sera iliyopo ya Tanzania ya sasa ni ya viwanda.


Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Dk.Kebwe Stephen Kebwe wakati akiwahimiza walimu na wanafunzi wa shule za sekondari Lubeho wilayani Gairo na kusisitiza kuwa bila kuwa na wataalamu wakiwemo wa ipo hatari dhana ya viwanda ikakosa mantiki iliyokusudiwa.

Alisema mkoa wa Morogoro umewekwa kama dira  ya utekelezwaja sera hiyo ambapo ili ikamilike lazima wanachi,walimu na wanafunzi kushirikiana kwa dhati ili kuwe na wataalamu mahususi watakao mudu teknolojia mpya inayohitaji uelewa wa sayansi.
“wazazi inatupasa kuwaboreshea watoto mazingira ya kusomea kama kuhakikisha madawati,vyumba vya madarasa na maabara vinakuwepo kuhuku walimu mkitakiwa kujitahidi kuwaelimisha watoto kwa bidii nao watoto kuwa wadadisi zaidi ili tupate wanasayansi bora” alisema Mkuu huyo wa mkoa.
Dk Kebwe amabye alilazimika kisitisha msafara wake kwa muda kuzungumza na wanachi walikuwa wamefurika shule ya sekondari ya Lubeho wakati akikagua vyumba vya madarasa,maabara na samani alisema endapo fulsa hiyo itachezewa na wanachi mkoani humo wasishangae kuwanufaisha wengine.
Aliwataka wanafunzi kusoma ya mchepuo wa Sayansi na kuyapenda masomo hayo likiwemo somo la Baiolojia, fizikia na kemia kwa kuwa ni rahisi isipokuwa uvivu wa wanafunzi ndi umekuwa chanzo cha kuyachukia na kuyakimbia.
“Masomo ya sayansi sio magumu kama wengine wanavyosema, ni masomo rahisi sana kuliko masomo mengine kama biashara na sanaa lakini pia sayansi ni maisha yetu tunayoishi nayo kila kukicha” alisema Dk.Kebwe. 
Aidha, aliwataka wanafunzi kupenda michezo kwa ajili ya kuuweka mwili kuwa mkakamavu wenye Afya hali itakayopelekea kiakili kufanya kazi kwa wepesi lakini pia kuongeza mahusiano mazuri baina ya wanafunzi hata walimu wao kupitia michezo.
Kwa upande wa madawati,  Mkuu huyo wa Mkoa aliutaka uongozi wa  Wilaya ya Gairo kusimamia suala nzima la ubora wa madawati yanayotengenezwa na kuagiza kuitisha kongamano la wadau wa Elimu wilayani humo ili kutafakari namna watakavyotekeleza agizo la Rais kabla ya Juni 30.
Hadi mwanzoni mwa mwezi Juni Wilaya ya Gairo ilikuwa inakabiliwa na upungufu wa samani 7,229 ikiwa ni pamoja na meza  960, viti 1,127 na madawati 5,142 samani ambazo hadi kukamilika kwake zitagharimu karibu shilingi 307 milioni.









No comments:

Post a Comment